Magavana wa Marekani wawasilisha orodha ya maswali kwa serikali kuu juu ya mpango wa chanjo ya COVID-19
(GMT+08:00) 2020-10-19 09:19:09
Shirikisho la Magavana la Taifa NGA jana Jumapili lilituma orodha ya maswali kwa serikali ya Trump likitaka ufafanuzi juu ya serikali kuu itakavyogawanya kwa ufanisi na kusimamia chanjo ya COVID-19.
Kwenye mkutano na wanahabari gavana wa jimbo la New York ambaye pia ni mwenyekiti wa NGA Andrew Cuomo amesema orodha ya maswali ambayo imewasilishwa na magavana wa nchi nzima kutoka vyama vya Republican na Democratic, inahusu fedha za usimamizi wa chanjo, njia ya ugawaji, na mawasiliano na mahitaji ya taarifa.
Amesema wameomba kukutana na rais ili kujadili namna itakavyofanya kazi baina ya serikali kuu na majimbo, kwani watahitajika kuwa tayari kujibu maswali yote kabla ya chanjo kupatikana ili muda utakapofika wa kuwapa chanjo watu asiwepo kiongozi ambaye hana uelewa juu ya utaratibu wa kutoa chanjo.