• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda yawakamata wasafiri wenye vyeti feki vya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-10-19 09:19:41

    Mamlaka ya afya ya Usafiri wa Anga ya Uganda jana iliwakamata wasafiri 24 wenye vyeti feki vya COVID-19 kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Entebbe.

    Msemaji wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Uganda Vianney Luggya amesema abiria hao walikamatwa baada ya kuonesha vyeti vyenye majibu feki ya COVID-19 wakati wakiingia uwanja wa ndege kwa ajili ya kusafiri maeneo mbalimbali. Hivi sasa abiria hao wamekabidhiwa kwa polisi wa usafiri wa anga ili kuchunguzwa na kujua walipata vipi vyeti hivyo feki, na baadaye kuwashtaki kwa makosa yoyote ambayo watakuwa wamekiuka.

    Luggya amewataka abiria kutoghushi vyeti vyenye majibu ya COVID-19 kwani amesema kuna utaratibu maalumu uliowekwa kwenye uwanja wa ndege ambao unatambua kama cheti ni halali au feki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako