• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapongezwa kwa uzoefu wake wa kupunguza umaskini

    (GMT+08:00) 2020-10-19 09:24:25

    Tarehe 17 ni siku ya taifa ya kuwasaidia maskini ya China na siku ya kutokomeza umaskini duniani. Takwimu zilizotolewa na Benki ya Dunia inaonesha kuwa, kwa mujibu wa kiwango cha kimataifa ambacho mtu anaishi chini ya dola 1.9 za Kimarekani kwa siku, katika miaka 40 iliyopita tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango, zaidi ya Wachina milioni 800 wameondokana na umaskini, idadi ambayo ni zaidi ya asilimia 70 ya watu wote walioondokana na umaskini duniani katika kipindi hicho. Baada ya kumaliza kazi ya kutokomeza umaskini uliokithiri mwaka huu, China inatarajiwa kutimiza lengo la kupunguza umaskini lililowekwa na Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya Mwaka 2030 ya Umoja wa Mataifa miaka 10 mapema kuliko ilivyopangwa.

    Je, kwa nini China imepata mafanikio makubwa namna hiyo katika kupunguza umaskini? Jibu ni kuwa China siku zote inachukulia maendeleo kama ni njia ya kimsingi ya kutatua tatizo la umaskini.

    Vilevile, wakati China inajitahidi kuondoa umaskini nchini humo, pia imeunga mkono na kusaidia nchi zinazoendelea haswa zile zilizo nyuma zaidi kimaendeleo kupunguza umaskini. China imependekeza kuanzishwa kwa Benki ya Maendeleo ya BRICS na Benki ya Uwekezaji wa Miundombinu ya Asia AIIB, na kujenga "Ukanda Mmoja, Njia Moja" pamoja na nchi mbalimbali, ili kuleta mazingira mazuri kwa juhudi za kukabiliana na umaskini za nchi zinazoendelea, kuzisaidia kujiunga na mlolongo wa kimataifa wa uzalishaji na utoaji wa bidhaa, na kuongeza uwezo wao wa kujiendeleza.

    Umoja wa Mataifa umekadiria kuwa, kutokana na athari ya janga la COVID-19, lengo la kupunguza umaskini la Ajenda yake ya Maendeleo Endelevu ya Mwaka 2030 halitaweza kutimizwa. Katika wakati huo wa taabu, uzoefu wa China katika kupunguza umaskini na ushirikiano kati yake na nchi nyingine ni muhimu sana. Katika siku za baadaye, China itaendelea kuzingatia suala la maendeleo, kuhimiza kufufuka kwa uchumi wa dunia, kupanua njia mpya ya mawasiliano na ushirikiano katika kupambana na umaskini duniani, na kutoa mchango wa Kichina kwa juhudi hizo .

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako