Tarehe 17 Oktoba ilikuwa ni Siku ya kuondoa Umaskini duniani. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres akitoa hotuba ameitaka jumuiya ya kimataifa kusimama bega kwa bega na watu wenye matatizo ya kiuchumi wakati wa janga la virusi vya Corona na baada ya kumaliza kwa janga hilo, na kutoa msaada wa lazima kwao.
Bw. Guterres pia amesema nchi mbalimbali zinatakiwa kuchukua hatua zenye nguvu kwa pamoja, kuharakisha mabadiliko ya muundo wa kiuchumi, na kuwekeza kwa ajili ya kufufuka kwa ukuaji wa uchumi endelevu ambao hautakuwa na uchafuzi wa mazingira.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |