• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ushiriki wa wanawake wa Afrika kwenye mambo ya kisiasa waongezeka

    (GMT+08:00) 2020-10-19 09:28:39

    Kamati ya Umoja wa Afrika imesema Afrika imepata maendeleo makubwa katika kuwashirikisha wanawake kwenye mambo ya kisiasa katika mwongo uliopita.

    Taarifa iliyotolewa na Umoja wa Afrika inasema kuwa, katika mwongo uliopita maendeleo makubwa yamepatikana katika kubadilisha ahadi kuwa utekelezaji, huku nchi nyingi za Afrika zikipiga hatua kubwa katika kuinua hadhi ya wanawake kupitia njia za sheria na katiba, mfumo wa kijinsia, pamoja na kuweka mazingira mazuri ya kuwawezesha wanawake.

    Umoja wa Afrika umesema mchakato wa ushiriki wa wanawake wa Afrika katika kutoa uamuzi wa kisiasa umeongezeka, ambapo nchi nne wanachama wake zimeorodheshwa kwenye nchi 10 duniani zenye idadi kubwa ya wanawake bungeni. Nchi hizo nne ni Rwanda, Namibia, Afrika Kusini na Senegal.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako