• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Huenda beki wa Liverpool akawa nje kwa msimu mzima kutokana na kujeruhiwa

    (GMT+08:00) 2020-10-19 17:58:54

    Beki wa Liverpool, Virgil van Dijk anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu baada ya kujeruhiwa gozi kwenye mechi iliyochezwa wikendi hii ikishuhudia Liverpool ikisimamishwa kwa sare ya 2-2 na Everton katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) uwanjani Goodison Park. Van Dijk alikumbana na gilikipa Jordan Pickford na ikabidi aondolewe uwanjaji katika dakika ya 11. Ingawa haijulikani atakuwa nje ya uwanja kwa muda gani, Liverpool wanahofua kwamba huenda nyota huyo akakosa mechi zote zilizosalia msimu huu. Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema Van Dijk ameumia sana na kua uwezekano kuwa hatakuwepo uwanjani kwa muda mrefu, na hilo litakuwa ni pigo kubwa kwa Liverpool. Van Dijik amewahi kuzichezea Celtic na Southampton na kuhamia Liverpool Januari 2018.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako