• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kocha mpya wa yanga aanza kazi, huku akikabiliwa na changamoto mbalimbali

    (GMT+08:00) 2020-10-19 18:00:04

    Kocha Mkuu wa Yanga Mrundi Cedric Kaze, tayari ameanza kukifanyisha mazoezi kikosi chake tayari kukiongoza kikosi hicho kukiwa na wingu la rekodi ya kutopoteza mechi yoyote ya mtangulizi wake, Mserbia Zlatko Krmpotic. Mbali rekodi ya kutopoteza mechi, pia kwenye mechi za kirafiki Mserbia huyo hakupoteza mchezo wowote kati ya michezo mitano ambayo aliiongoza timu hiyo, kwa kushinda minne na kutoka sare mmoja. Hivyo Kaze ambaye alitua Yanga Alhamisi ya wiki iliyopita, amenza kazi ya kuifundisha Yanga ikiwa katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi kwa pointi 13 ,sawa na Simba iliyopo nafasi ya pili kutokana na kuizidi kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa. Kaze amesemaa ana uhakika mashabiki wa timu hiyo watafurahia soka la burudani na ushindani, huku akihitaji muda kuweza kukiunganisha kikosi hicho. Changamoto yake ya kwanza itakuwa dhidi ya Polisi Tanzania katika Uwanja wa Mkapa Alhamisi wiki hii, na siku tatu baadaye itakutana na KMC FC kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako