• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • EPL: Westham yatoka nyuma kufungwa magoli na matatu na kupata sare dhidi ya Tottenham

    (GMT+08:00) 2020-10-19 18:01:24

    Kocha Mkuu wa Tottenham Hotspur, Jose Mourinho, amesema waliadhibiwa jana mbele ya West Ham United kwa kuamini kwamba wamemaliza kazi jambo lililowaponza wagawane pointi mojamoja. Mchezo huo wa Ligi Kuu England uliochezwa Uwanja wa Tottenham Hotspur, ulikamilika kwa timu zote kufungana mabao 3-3 huku West Ham wakipindua meza zikiwa zimebaki dakika 8 mpira kumalizika kwa kuwa walikuwa wamefungwa mabao matatu mpaka dakika ya 81. Spurs ilianza kufunga dakika ya kwanza kupitia kwa Son Heung-min na Harry Kane alitupia mawili dakika ya 8 na 16 na meza ilianza kupinduka katika dakika ya 82 kupitia kwa Fabian Balbuena na dakika ya 85 Davinson Sanchez alijifunga huku lile la mwisho likifungwa na Manuel Lanzini katika dakika ya 90+4 na kufanya ubao usome 3-3. Inawezekana kuwa hii ni siku ya ajabu kabisa na kushangaza kwa Jose Mourinho tangu aanze kufundisha soka, na mwenyewe amelalamikia kujiamini kupita kiasi kwa wachezaji wake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako