• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Lawrence Juma awagonganisha Cor Mahia na Sofapaka ligi kuu Kenya

    (GMT+08:00) 2020-10-19 18:01:55

    Klabu za Gor Mahia na Sofapaka za kenya zinaendelea na ugomvi juu ya uhamisho wa hivi karibuni wa Lawrence Juma. Kiungo huyo wa kimataifa alihama kutoka Gor Mahia kwenda Sofapaka Ijumaa katika mazingira ya kutatanisha. Mabingwa wa Kenya wamethibitisha kuwa wameliandikia barua Shirikisho la Soka la Kenya likisema Sofapaka wamemnasa mchezaji huyo bila kufuata taratibu zilizowekwa. Meneja wa timu ya K'Ogalo, Jolawi Obondo, amesema walishtushwa na hatua hiyo ikizingatiwa kuwa mkataba wa Juma unamalizika Desemba 31 mwaka huu. Lakini katika hali ya kushangaza mwenyekiti wa Sofapaka Elly Kalekwa alipinga mchezaji huyo wa Harambee Stars alijiunga nao kwa uhamisho wa bure. Juma kijana mwenye umri wa miaka 27, alikuwa akifanya mazoezi ya mapema ya msimu huu na Gor huku uvumi juu ya yeye kuondoka ukienea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako