• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Floyd Mayweather aendelea na vituko vyake na pesa

    (GMT+08:00) 2020-10-19 18:04:42

    Bondia mstaafu wa Marekani Floyd Mayweather anatajwa kuwa alijikusanyia si chini ya dola bilioni 1 kutokana na mapambano yake ulingoni. Imefahamika kuwa bondia huyo ni mpenda anasa na anatumia pesa nyingi kuishi maisha ya kifahari. Mayweather, ambaye alistaafu kwa ushindi wa mapambano 50 bila kushindwa (ikiwa ni pamoja na 27 KOs), anatajwa kuwa na mkusanyiko wa magari katika maeneo mawili tofauti, na moja liko Las Vegas na lingine Los Angeles. Hivi karibuni alifungua gereji yake na baadhi ya watu waliofanikiwa kupiga picha ya magari yake huko Las Vegas na kuiweka kwenye Instagram. Mkusanyiko wa magari yake umwashangaza mashabiki wake, ikiwa ni pamoja na nyota wa Juventus Cristiano Ronaldo, aliyevutiwa na magari hayo. Mkusanyiko wa Las Vegas una idadi kubwa ya Rolls-Royces.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako