• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hali ya kufufuka kwa uchumi wa China iliimarika zaidi katika robo ya tatu ya mwaka huu

    (GMT+08:00) 2020-10-19 18:50:26

    Katika robo ya tatu ya mwaka huu kasi ya ufufukaji wa uchumi wa China iliendelea kuongezeka kutokana na shughuli mbalimbali kurejea katika hali ya kawaida na udhibiti wenye ufanisi wa maambukizi ya virusi vya Corona.

    Idara ya takwimu ya taifa imesema pato la ndani la taifa katika kipindi hicho (Q3) liliongezeka kwa asilimia 4.9, likiwa ni zaidi kuliko asilimia 3.2 za robo ya pili (Q2). Katika robo hizo tatu ongezeko la jumla lilikuwa kubwa zaidi kwa asilimia 0.7 mwaka hadi mwaka, likileta ongezeko baada ya kupungua kwa asilimia 1.6 katika nusu ya kwanza ya mwaka huu na asilimia 6.8 katika robo ya kwanza.

    Katika robo ya tatu viashiria vikuu vimeonyesha kurudi kwenye hali chanya, huku uzalishaji viwandani ukiongezeka kwa asilimia 5.8 na biashara ya rejareja ikiongeza kwa mara ya kwanza, kwa asilimia 0.9 ya mwaka hadi mwaka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako