• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Sudan yaamua kuongeza nafasi tatu kwenye baraza la utawala

    (GMT+08:00) 2020-10-19 18:50:47

    Baraza la utawala la Sudan na Baraza la mawaziri la nchi hiyo wameamua kuongeza nafasi tatu zaidi kwenye baraza hilo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa makubaliano ya amani yaliyosainiwa Oktoba 3.

    Taarifa iliyotolewa na baraza hilo imesema mkutano wa pamoja umeidhinisha makubaliano yaliyosainiwa mjini Juba Oktoba 3 kwa nyaraka ya kikatiba, na kuongeza nafasi hizo tatu ni uamuzi muhimu zaidi kupitishwa na mkutano huo. Kuongezwa kwa viti hivyo vitatu kunafanya baraza la utawala la nchi hiyo kuwa na viti 14.

    Makubaliano ya Oktoba 3 mjini Juba yalisainiwa kati ya serikali na makundi yenye silaha, yakiwa na itifaki mbalimbali ikiwa ni pamoja na mambo ya usalama, kugawana madaraka na utajiri, kuwafidia wakimbizi, umiliki wa ardhi na kuleta haki na maendeleo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako