Kamati kuu ya ya kuzuia na kudhibiti majanga ya asili ya Vietnam, imesema kuwa mafuriko, maporomoko ya ardhi na majanga mengine ya asili yanayotokana na mvua kubwa yamesababisha vifo vya watu 90 na wengine 34 hawajulikani walipo kwenye majimbo ya kati ya Vietnam katika wiki mbili zilizopita.
Ripoti iliyotolewa hivi karibuni na kamati hiyo, inasema wengi wa watu walioripotiwa kufa wako katika majimbo ya Quang Tri, Thua Thien Hue na Quang Nam. Maafa hayo pia yamesababisha kuharibika kwa barabara kuu kadhaa za kitaifa na za mitaa kwenye majimbo hayo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |