• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa China kuhudhuria mkutano Baraza la Usalama la UM kuhusu hali ya eneo la Ghuba

    (GMT+08:00) 2020-10-19 20:29:44

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian amesema, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jumanne litafanya mkutano wa ngazi ya mawaziri kuhusu hali ya eneo la Ghuba kwa njia ya mtandao, waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi atahudhuria mkutano huo.

    Bw. Zhao alipoulizwa swali kuhusu juhudi za kupunguza umaskini duniani, amesema mafanikio yaliyopatikana na China katika kupunguza umaskini ni muhimu kwa dunia, na imechangia juhudi za kupunguza umaskini duniani.

    Tarehe 17 ilikuwa siku ya kutokomeza umaskini duniani, na pia ni siku ya 7 ya kuwasaidia watu maskini nchini China. Bw. Zhao amesema umaskini ni changamoto ya binadamu wote, na kutokomeza umaskini ni lengo la kwanza la Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya Mwaka 2030 ya Umoja wa Mataifa.

    Amesema katika miaka 40 iliyopita tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango, zaidi ya Wachina milioni 800 wameondokana na umaskini, na mwaka huu China itatimiza lengo la kutokomeza umaskini vijijini. Ameongeza kuwa wakati huo huo China imezisaidia nchi zinazoendelea kupunguza umaskini kadiri iwezavyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako