• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • AfCFTA yaweza kunufaika uzoefu wa COMESA

    (GMT+08:00) 2020-10-20 09:03:05

    Eneo la Biashara Huria la Afrika AfCFTA linaweza kunufaika na uzoefu wa soko la pamoja la Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika COMESA katika biashara huria.

    Akiongea kwenye mkutano kwa njia ya mtandao, mkurugenzi wa kitengo cha mafungamano ya kikanda na biashara cha Kamati ya Uchumi ya Afrika katika Umoja wa Mataifa UNCA Stephen Karingi amesema kwa AfCFTA, COMESA ni jumuiya ya lazima na muhimu kiujenzi, iliyopiga hatua katika maeneo muhimu ya mafungamano ambayo AfCFTA inaweza kujifunza. Aidha amesema eneo hili pia linaweza kunufaika na uzoefu wa COMESA katika kujenga taasisi za uungaji mkono, kama vile maeneo ya fedha za biashara, bima ya biashara, mifumo ya malipo ya kikanda na mazingira ya utawala rahisi wa biashara.

    Karingi ameeleza kuwa utekelezaji wa mafanikio wa AfCFTA utategemea na jumuiya za uchumi za kikanda RECs, katika kuinua mafanikio na pia kujifunza na kuepuka mitego na changamoto zinazowakabili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako