• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya kuanza kurejesha huduma za treni ya SGR kutoka Nairobi hadi viungani

    (GMT+08:00) 2020-10-20 09:03:28

    Shirika la Reli la Kenya KRC limetangaza kuwa kuanzia kesho Jumatano Wakenya watatumia usafiri wa treni ya SGR kutoka Nairobi hadi kwenye viunga vya kaskazini magharibi vya mji huo mkuu.

    Shirika hilo limesema huduma za usafiri wa Madaraka Express katika vituo vya Ngong, Ongata Rongai kutoka Kituo cha Nairobi zitaanza Oktoba 21. Usafiri wa masafa marefu kutoka Nairobi hadi Suswa pia utarejeshwa ambao utakuwa kila siku za Jumatano, Ijumaa na Jumapili. Urejeshwaji wa huduma za usafiri wa treni ambazo zilisitishwa mwezi Aprili kufuatia mlipuko wa COVID-19 utakamilisha urejeshwaji mzima wa huduma za SGR kwa abiria nchini humo. Mahitaji ya abiria za SGR yameongezeka nchini Kenya tangu mwezi Julai baada ya kuanza kurejeshwa tena huduma hizo taratibu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako