• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaiunga mkono Ethiopia kupambana na COVID-19 na nzige wa jangwani

    (GMT+08:00) 2020-10-20 09:03:56

    Afisa ubalozi anayeshughulikia mambo ya uchumi na biashara kwenye ubalozi wa China nchini Ethiopia Liu Yu amesema serikali ya China imeazimia kuiunga mkono Ethiopia katika kupambana na janga la COVID-19 pamoja na uvamizi wa nzige wa jangwani.

    Bi Liu amesema hayo wakati akiikabidhi Ethiopia vifaa vya kupambana na nzige, vikiwemo tani 72 za dawa za kuulia wadudu, dawa za kupuliza kwa mkono zipatazo 2,000 pamoja na seti 20,00 za vifaa vya kujikinga.

    Amebainisha kuwa mwaka huu ni muhimu sana duniani, hasa kwa Ethiopia ambayo ni nchi inayosumbuliwa na sio janga la COVID-19 pekee bali hata uvamizi mbaya wa nzige wa jangwani ambao haujawahi kushuhudiwa kwa miaka 25. Hivyo amesema China imekuwa nchi ya kwanza kutoa vifaa vya matibabu na kupeleka timu ya watumishi wa afya kuisaidoa nchi hiyo kupambana na COVID-19.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako