Shirika la Takwimu la Ulaya Eurostat limeripoti kuwa, wakati janga la COVID-19 linapoenea barani humo, vifo vya watu 168,000 vimerekodiwa kwenye Umoja wa Ulaya kuanzia tarehe 2 Machi hadi tarehe 2 Juni mwaka huu.
Takwimu hizo zimeonesha kuwa, vifo vya watu vilikuwa chini ya kiwango cha wastani cha mwaka 2016-2019, lakini vilianza kuongezeka katika wiki ya tisa na kumi, vikizidi kiwango cha wastani tokea wiki ya 11, na kufikia kilele katika wiki ya 14 ikiwa na vifo vya watu 36,000.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |