• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Biashara kati ya Guangdong na Afrika yaongezeka kwa asilimia 30 kila mwaka

    (GMT+08:00) 2020-10-20 09:35:13

    Serikali ya mji wa Guangzhou jana ilifanya mkutano na waandishi wa habari kuhusu biashara kati ya China na Afrika na kutangaza kuwa China imekuwa mwenzi mkubwa wa kwanza wa kibiashara wa Afrika kwa miaka 11 mfululizo, na haikusitia kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona.

    Vile vile thamani ya biashara kati ya mkoa wa Guangdong, China na Afrika imechukua asilimia 25 ya thamani ya jumla ya biashara kati ya China na Afrika, kiasi ambacho kimeongezeka kwa wastani wa asilimia 30 kila mwaka katika zaidi ya miaka 10 iliyopita.

    Habari zinasema kuwa, katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, kutokana na athari ya pamoja ya maambukizi ya virusi vya Corona, kushuka kwa bei ya mafuta ya kimataifa na maafa ya nzige katika Afrika Mashariki, ushirikiano wa kibiashara kati ya China na Afrika umekumbwa na shinikizo kubwa.

    Naibu mkuu wa shirikisho kuu la wafanyabiashara la Guangdong barani Afrika Bw. Huo Jiangtao amesema, China na Afrika wanaposhikamana kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona, mawasiliano ya uchumi na biashara kati ya Guangdong na Afrika hayajasita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako