Ndege ya kwanza ya abiria iliyotoka Falme za Kiarabu UAE imetua jana nchini Israel, takriban mwezi mmoja baada ya nchi hizo mbili kusaini makubaliano ya kurejesha safari kama kawaida.
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya uchukuzi ya Israeli imesema, nchi hizo mbili zinapanga kutia saini makubaliano rasmi Jumanne, ambapo ndege 28 za kibiashara kati ya Tel Aviv na Abu Dhabi au Dubai zitaweza kusafiri kila wiki.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |