Rais Donald Trump wa Marekani jana alisema, Marekani itaiondoa Sudan kwenye orodha ya "nchi zinazounga mkono ugaidi" baada ya kupokea malipo ya fidia ya Sudan.
Rais Trump amebainisha kuwa, Sudan imekubali kutoa dola za kimarekani milioni 335 kwa waathirika wa ugaidi na jamaa zao nchini Marekani, hivyo Marekani itaiondoa nchi hiyo kwenye orodha ya "nchi zinazounga mkono ugaidi" baada ya kupata pesa hizo.
Vyombo vya habari vya Marekani vimewanukuu maofisa wa Marekani kuwa, baada ya Sudan kuondolewa kwenye orodha hiyo, Sudan na Israel huenda zitatimiza uhusiano wa kawaida ndani ya siku kadhaa zijazo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |