Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO Bw. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema, hivi sasa, nchi 184 zimejiunga na mpango wa WHO wa matumizi sawa ya chanjo ya virusi vya Corona COVAX.
Bw. Ghebreyesus amesema, mpango huo ni mzuri zaidi duniani katika kusambaza kwa haki chanjo salama na yenye ufanisi zaidi duniani. Kusambaza chanjo hiyo kwa usawa ni njia yenye ufanisi zaidi na ya haraka zaidi ya kuhakikisha usalama wa watu wenye hatari zaidi ya kuambukizwa, kulinda utulivu wa mfumo wa afya duniani na kuharakisha kufufua uchumi wa dunia.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |