• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Ulaya na Uingereza zakubali kuongeza mazungumzo

    (GMT+08:00) 2020-10-20 09:51:09

    Kamati ya pamoja ya Uingereza na Umoja wa Ulaya imefanya mkutano wa nne na kujadiliana mustakabali wa uhusiano kati ya pande hizo mbili.

    Taarifa iliyotolewa na kamati hiyo imesema, pande hizo mbili zinahitaji kutumia nguvu zote kutatua tofauti zilizopo na kufikia makubaliano ili kuepusha Uingereza kujitoa kwenye umoja huo bila ya makubaliano yoyote.

    Taarifa hiyo pia imesema, kutimiza lengo hilo kunahitaji jitihada zisizo za kawaida. Pande hizo mbili zimekubali kuongeza mawasiliano ya kila ngazi, ikiwemo kufanya mkutano tena wa kamati hiyo katikati mwa mwezi ujao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako