• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchunguzi waonesha mkoa wa Xinjiang unatilia maanani suala la ajira kwa watu wa makabila madogomadogo

    (GMT+08:00) 2020-10-20 17:16:48

    Kituo cha Utafiti wa Maendeleo ya Xinjiang leo kimetoa ripoti ya uchunguzi kuhusu kazi na ajira kwa watu wa makabila madogomadogo mkoani Xinjiang. Uchunguzi unaonesha kuwa mkoa wa Xinjiang unatilia maanani suala hilo, na kuheshimu nia na hiari yao ya kufanya kazi na kutafuta ajira.

    Hivi karibuni baadhi ya majopo ya washauri bingwa ya nchi za magharibi yametoa ripoti yakidai kuwa watu wengi mkoani Xinjiang wanafanya kazi za kulazimishwa. Ili kutafuta ukweli wa suala hilo, Kituo cha Utafiti wa Maendeleo ya Xinjiang kiliwaalika wataalamu kushiriki kwenye uchunguzi kuhusu hali ya kazi na ajira za watu wa makabila madogomadogo mkoani humo.

    Timu ya uchunguzi iliyoundwa na kituo hicho ilitembelea miji ya Ili, Karamay na Kaxgar, pamoja na kampuni, vyama vya ushirika na vituo vya ujasiriamali zaidi ya 70 katika miji ya Beijing na Tianjin, na kufanya mahojiano na maofisa wa usimamizi, wafanyakazi, wanaojiajiri na watu wa makabila madogomadogo zaidi ya 8,000. Uchunguzi wao unaonesha kuwa, mkoa wa Xinjiang, kwa kushirikiana na miji mingine, serikali za ngazi mbalimbali na makampuni husika, umejitahidi kuwasaidia watu wa makabila madogomadogo kushiriki kwenye kazi na kutafuta ajira, umehakikisha haki za kufanya kazi na kujiendeleza za watu wa makabila mbalimbali zinatekelezwa, na watu wa makabila yote wanafanya kazi kwa hiari, kuchagua ajira zao wenyewe na kuanzisha biashara zao kwa uhuru, kwa hiyo shutuma zilizotolewa na majopo ya washauri bingwa ya nchi za magharibi si sahihi na hazina msingi wala ushahidi wowote.

    Takwimu zinaonesha kuwa kuanzia mwaka 2014 hadi 2019, mkoa wa Xinjiang ulitoa mafunzo ya ufundi stadi kwa watu wapatao milioni saba, miongoni mwao watu wapatao laki 3.8 wamejiingiza kwenye ujasiriamali na kuanzisha biashara zao na wengine zaidi ya laki 8.2 wamepata ajira. Katika kipindi hicho, kila mwaka wastani wa watu milioni 2.76 wa maeneo ya vijijini mkoani Xinjiang waliondoka nyumbani na kwenda kutafuta ajira nje ya mkoa huo.

    Ripoti hiyo pia inasema, mkoa wa Xinjiang umetimiza lengo la kuhakikisha watu wa makabila madogomadogo mkoani humo wanafanya kazi kwa uhuru, haki, usalama na heshima, hatua ambayo ni alama wazi ya maendeleo ya shughuli za haki za binadamu mkoani Xinjiang, na pia imethibitisha ufanisi wa sera madhubuti zilizowekwa na serikali kuu ya China kuhusu Xinjiang.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako