• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Usajili kwa ajili ya michezo ya Rock City Marathon 2020 waanza

    (GMT+08:00) 2020-10-20 17:33:38

    Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw. John Mongella, amezindua usajili wa mbio za Rock City Marathon huku akitoa wito kwa wadau mbalimbali wa Kanda Ziwa kushiriki kikamilifu katika kufanikisha mbio hizo. Mbio hizo zinatarajiwa kufanyika Novemba 29, mwaka huu eneo la Rock City Mall jijini Mwanza. Bw. Mongella amewaomba wadau mbalimbali wakiwamo washiriki na wadhamini kujitokeza kwa wingi, ili kuunga mkono mbio hizo zenye agenda ya kutangaza utalii wa ndani katika mikoa ya Kanda ya Ziwa. Katika hafla hiyo ambayo pia ilishuhudiwa na viongozi mbalimbali waandamizi wakijisajili kwa ajili kushiriki katika mbio hizo, Bw Mongella a alisisitiza ushiriki wa wadau kutoka Kanda ya Ziwa hususan katika Mkoa wa Mwanza kwa sababu hizi ni mbio zetu haitapendeza sana kuona wadau wakuu wa mbio hizi wakiwamo wadhamini na hata washiriki wanatoka kwa wingi mikoa iliyo nje ya Kanda ya Ziwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako