• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Rwanda yasema hatua za kinga na uungaji mkono wa umma vyachangia kupungua kwa maambukizi mapya ya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-10-20 18:34:09

    Waziri wa nchi anayeshughulikia afya ya msingi wa Rwanda Bw. Tharcise Mpunga amesema hatua mbalimbali za kinga na uungaji mkono vimechangia kupungua kwa maambukizi mapya ya virusi vya Corona.

    Baada ya ongezeko la maambukizi lililotokea katikati ya mwezi Agosti, mwezi huu idadi ya watu wanaoripotiwa kuambukizwa virusi hivyo imepungua, na hadi kufikia jumatatu idadi ya watu walioambukizwa ilikuwa 4,992, idadi ya waliopona ni 4797, na 34 wamefariki dunia.

    Bw. Mpunga amesema hatua muhimu zilizochangia kupungua kwa maambukizi mapya ya ugonjwa huo ni pamoja na kufuatilia watu wanaoshukiwa kuambukizwa, kupima, umbali wa kijamii, kufunga biashara na zuio la watu kutoka nje usiku.

    Hata hivyo licha ya mafanikio hayo Bw. Mpunga amesema ni mapema kusema Rwanda imeshinda mapambano dhidi ya COVID-19.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako