• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maandamano nchini Nigeria yachochea maambukizi ya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-10-20 18:34:32

    Wakati maelfu ya Wanigeria wakiandamana kupinga mauaji ya bila kufuata sheria na ukatili wa polisi, mwenyekiti wa kikosi kazi cha Ikulu cha kupambana na maambukizi ya COVID-19 Bw. Boss Mustapha ameonya kuwa mikusanyiko mikubwa inaweza kuongeza kasi ya maambukizi ya ugonjwa huo.

    Ofisa huyo amesema hayo kufuatia kupuuzwa kwa njia za kujikinga kulikooneshwa na maelfu ya wananchi wanaondamana kwenye kampeni inayoendelea katika nchi nzima. Watu hao wamekuwa wakiandamana kupinga ukatili ulioripotiwa kufanywa na kikosi maalumu cha polisi cha kupambana na ujambazi kilichovunjwa hivi karibuni. Kwenye mikusanyiko hiyo watu hawavai barakoa, hawaweki umbali kati yao na kutozingatia usafi.

    Kwa mujibu wa CDC ya Nigeria hadi sasa watu zaidi ya elfu 68 wameambukizwa, na jumatatu kulikuwa na maambukizi mapya 118.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako