• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China haiwajibiki na tatizo la madeni la baadhi ya nchi

    (GMT+08:00) 2020-10-20 19:16:48

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian amesema, tatizo la madeni ya baadhi ya nchi linatokana na nchi zilizoendelea ikiwemo Marekani na mashirika ya kimataifa ya kifedha, na China haipaswi kuwajibika na tatizo hilo.

    Bw. Zhao amesema China haijawahi kuzilazimisha nchi zenye tatizo la madeni kulipa madeni, badala ya kufanya hivyo, inadumisha mawasiliano na majadiliano na nchi hizo, na hata kusamehe baadhi ya madeni yao. Ameongeza kuwa China imeshiriki kwenye pendekezo la Kundi la Nchi 20 la kuziruhusu nchi zilizoko nyuma kimaendeleo zaidi, kuchelewa kulipa madeni, ili kupunguza athari za janga la COVID-19 kwa uchumi wa dunia na wa nchi mbalimbali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako