• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe wa China aihimiza Jamhuri ya Afrika ya Kati ifanye uchaguzi kwa wakati uliopangwa

    (GMT+08:00) 2020-10-20 19:37:46

    Naibu mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Dai Bing jana kwenye mkutano wa Baraza la Usalama kuhusu hali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati alisema kuwa Jamhuri ya Afrika ya Kati inatakiwa kufanya uchaguzi wa rais na wabunge kwa wakati uliopangwa.

    Balozi Dai alisema huu utakuwa ni uchaguzi wa kwanza tangu makubaliano ya amani ya Jamhuri ya Afrika ya Kati yasainiwe, ambao una umuhimu mkubwa katika kuimarisha mchakato wa amani. Serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati imeondoa matatizo na changamoto nyingi na kufanya juhudi kufanya maandalizi kwa ajili ya uchaguzi huo. Amesema anaamini kuwa pande zote za nchi hiyo zitaendelea kuhimiza maandalizi ya uchaguzi kwa utaratibu na kufanya uchaguzi kwa wakati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako