• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yatoa wito wa kuongeza juhudi katika kupambana na magonjwa mengine katika Afrika na si COVID-19 pekee

    (GMT+08:00) 2020-10-21 09:21:58

    Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameitaka jamii ya kimataifa kutoruhusu mapambano dhidi ya COVID-19 kuingilia juhudi za kutokomeza malaria, polio, Ukimwi, kifua kikuu na magonjwa mengine katika Afrika.

    Akiongea kwenye mkutano wa Mwaka wa Baraza la Kutokomeza Malaria uliofanyika kwa njia ya mtandao Jumatatu jioni ambao umeitishwa na Mfuko wa Bill and Melinda Gates, Kenyatta amesema habari za mafanikio na mafunzo kutokana na mwitikio wa dunia juu ya COVID-19 zinapaswa kuunganishwa na kutumiwa katika vita dhidi ya magonjwa haya ili kuharakisha utokomezaji wake.

    Amesema mapambano dhidi ya malaria katika Afrika yamekuwa yakitupwa mkono na mataifa yaliyoendelea na washirika wengi huku nchi na mashirika yakielekeza rasilimali zao kwenye janga lililopo la COVID-19.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako