• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan yamhakikishia Mwendesha mashtaka wa ICC kwamba wahanga wa mgogoro wa Darfur watapatiwa haki yao

    (GMT+08:00) 2020-10-21 09:22:24

    Mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai ICC Fatou Bensouda amesema amehakikishiwa na serikali ya Sudan kwamba wahanga wa mgogoro wa Darfur watapatiwa haki yao na kuwawajibisha wahusika wote wa uhalifu.

    Bensouda amesema hayo baada ya kukutana na mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Sudan Abdel Fattah Al-Burha katika Ikulu ya rais mjini Khartoum. Ameeleza kuwa wakati wa mkutano wake alihisi utayari na nia ya maofisa wa Sudan kuipa ushirikiano ICC na kutafuta njia nzuri ya kufikia ushirikiano.

    Bi. Bensouda ameendelea mbele kwa kusema ziara yake hii sio ya mwisho bali ni mwanzo wa juhudi za kutafuta ushirikiano kati ya Sudan na ICC ili kutimiza haki kwa wahanga wa vita vya Darfur.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako