• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Ulaya watoa msaada mpya wa EURO milioni 43 kwa nchi tatu za katikati ya sehemu ya Sahel

    (GMT+08:00) 2020-10-21 09:26:37
    Umoja wa Ulaya watoa msaada mpya wa EURO milioni 43 kwa nchi tatu za katikati ya sehemu ya Sahel

    Wakati hali ya kibinadamu kwenye sehemu ya Sahel barani Afrika inapozidi kuwa mbaya, Umoja wa Ulaya umetangaza kutoa msaada wa fedha EURO milioni 43, sawa na dola milioni 50 za kimarekani, kwenye nchi za Mali, Niger na Burkina Faso, ili kuzisaidia zikabiliane baa la njaa.

    Taarifa iliyotolewa na Kamati ya Umoja wa Ulaya imeonesha kuwa, EURO milioni 24, sawa na dola milioni 28 za kimarekani, zitatumiwa katika operesheni za kibinadamu katika nchi hizo tatu, nyingine EURO milioni 20, sawa na dola milioni 24 za kimarekani zitatumiwa katika kulisaidia Shirika la Mpango wa Chakula duniani WFP.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako