• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Israel na UAE zafikia makubaliano manne

    (GMT+08:00) 2020-10-21 10:14:18

    Ofisi ya Wizara ya mambo ya nje ya Israel jana ilitoa taarifa ikisema kuwa, waziri mkuu wa nchi hiyo Bw. Benjamin Netanyahu amekutana na ujumbe wa Umoja wa Falme za Kiarabu UAE, ambapo wamefikia makubaliano manne kati ya pande hizo mbili.

    Taarifa inasema, Israel na UAE zimefikia makubaliano kuhusu uhifadhi wa uwekezaji, kumbukumbu kuhusu teknolojia ya kisayansi, mkataba kuhusu safari za anga na makubaliano ya kusameheana vita.

    Bw. Netanyahu amesema, makubaliano hayo yameweka msingi kwa ajili ya ushirikiano wa kibiashara na hali ya kunufaishana kati ya nchi hizo mbili, na yataleta matokeo halisi kwa watu wa nchi hizo mbili.

    Waziri wa nchi wa mambo ya fedha wa UAE Obaid Humaid Al-Tayer amesema makubaliano hayo yataimarisha uhusiano kati yao na ushirikiano wa uchumi kati ya nchi hizo mbili utapata matokeo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako