• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ripoti ya UN yaonesha kuwa bado kuna safari ndefu ya kutimiza usawa wa kijinsia

    (GMT+08:00) 2020-10-21 10:19:50

    Ripoti iliyotolewa jana na Umoja wa Mataifa kuhusu wanawake imeonesha kuwa, hadi sasa hakuna nchi yoyote iliyofanikiwa kutimiza usawa wa kijinsia, na bado kuna safari ndefu sana ya kutimiza usawa wa kijinsia duniani.

    Kwa mujibu wa ripoti ya "Wanawake Duniani Mwaka 2020: Mwelekeo na Takwimu", chini ya asilimia 50 ya wanawake wenye umri wa kufanya kazi wako kwenye soko la ajira, na takwimu hizo hazijabadilika katika miaka 25 iliyopita.

    Ripoti hiyo pia imeonya kuwa, maambukizi ya COVID-19 yameathiri zaidi kazi na maisha ya wanawake, wanawake hushughulikia kazi za nyumbani na huduma za utunzaji bila malipo, na uwezo wao wa kiuchumi umezuiliwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako