• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KENYA: HOFU ETHIOPIA IKIANZA KUUZA KIRAA SOMALIA

    (GMT+08:00) 2020-10-21 17:37:46

    Wakuzaji miraa nchini Kenya wameeleza wasiwasi kwamba huenda wakapoteza soko la Somalia kabisa, baada ya Ethiopia kuanza kusafirisha zao hilo nchini humo.

    Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari katika taifa hilo, shirika la ndege la Ethiopia, liliwasilisha shehena ya kwanza ya zao hilo katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Aden Adde, Mogadishu mnamo Jumamosi.

    Hali hiyo imezua wasiwasi mkubwa miongoni mwa wakuzaji hao nchini, ikizingatiwa ndio wamekuwa wakidhibiti mauzo ya zao Somalia kwa muda mrefu.

    Wakuzaji miraa nchini Ethiopia wamekuwa wakidhibiti soko la Hargeisa. Wakenya walishindwa kupenya soko hilo kutokana na kiwango cha juu cha kodi.

    Vyombo hivyo viliripoti kwamba serikali ya Somalia imeiruhusu Ethiopia kuendesha biashara hiyo nchini humo, huku marufuku dhidi ya Kenya ikiendelea kuwepo.

    Mwenyekiti wa Chama cha Wakuzaji Miraa cha Nyambene (Nyamita), Bw Kimathi Munjuri, alisema kuwa serikali ya Somalia pia imeimarisha usalama katika Bara Hindi kuhakikisha hakuna miraa kutoka Kenya inaingizwa nchini humo.

    Mwenyekiti wa Chama cha Wakuzaji Miraa wa Maua, Bw Mohamed Quresh, alisema serikali ya Somalia pia ilitoa makataa ya siku tatu kwa wafanyabiashara kutoka Kenya ambao wamekuwa wakiingiza zao nchini humo kupitia Mandera kukoma kufanya hivyo mara moja.

    Bw Munjuri aliiomba serikali ya Kenya kufanya mazungumzo na Somalia ili kuwarejeshea udhibiti wa soko hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako