• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchumi wa China wadumisha mwelekeo mzuri wa kufufuka

    (GMT+08:00) 2020-10-21 18:01:36

    Takwimu zilizotolewa jumatatu na serikali ya China zinaonesha kuwa, katika robo tatu za mwanzo za mwaka huu, Pato la Ndani la China (GDP) liliongezeka kwa asilimia 0.7 ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hiki. Katika robo ya pili na ya tatu ya mwaka huu, uchumi wa China ulikua kwa asilimia 3.2 na asilimia 4.9 mtawalia. Takwimu hizo zimefuatiliwa sana na vyombo vya habari vya kimataifa.

    Shirika la utangazaji la Marekani CNN limeripoti kuwa ukuaji wa asilimia 4.9 wa uchumi wa China katika robo ya tatu ya mwaka huu umeonesha mwelekeo mzuri wa ufufukaji baada ya janga la virusi vya Corona kudhibitiwa nchini China, hasa wakati huu ambapo nchi nyingine bado zimekwama kwenye msukosuko wa kiuchumi unaotokana na janga hilo, China imekuwa nchi pekee kote duniani inayoshuhudia ufufukaji wa kasi wa uchumi.

    Gazeti la Financial Times la Uingereza limechapisha makala ikisema ukuaji mzuri wa Pato la Ndani na matumizi katika robo ya tatu ya mwaka huu nchini China, utatoa msukumo mkubwa kwa ufufukaji wa uchumi wa China baada ya janga la virusi vya Corona.

    Gazeti la Wallstreet Journal la Marekani limebainisha kuwa janga la virusi vya Corona lilitoa pigo kubwa kwa uchumi wa China katika nusu ya mwaka iliyopita, na hivi sasa ufufukaji endelevu wa uchumi wa China umethibitisha nguvu kubwa ya uchumi wa China, na kwa upande wa viashiria vikuu vya kiuchumi ikiwemo ajira, matumizi, uagizaji na uuzaji nje, uchumi wa China unafufuka kwa kasi zaidi kuliko nchi nyingine.

    Shirika la habari la Marekani AP linaona hatua kali za udhibiti wa maambukizi ya virusi vya Corona zimeweka mazingira mazuri kwa ajili ya ukuaji wa uchumi wa China, na ufufukaji wa uchumi wa China unazidi kupanuka na utegemezi wake kwa hatua za vichocheo za serikali pia unaendelea kupungua.

    Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC limesema, Wiki ya mapumziko ya Siku ya Taifa ya China mwaka huu ni mfano mmoja tu wa ufufukaji wa haraka wa uchumi wa China. Kutokana na zuio la usafiri wa kimataifa, wachina wengi wameanza kukumbatia safari za ndani ya nchi, na hivyo kuongeza kidhahiri idadi ya watalii wa ndani na mapato yanayotokana na sekta ya utalii katika kipindi hicho.

    Gazeti la New York Times la Marekani limetoa ripoti ikisema wakati ambapo Marekani na Ulaya zinakabiliwa na wimbi la pili la maambukizi ya virusi vya Corona, katika miezi kadhaa ijayo, uchumi wa China utazidi kutangulia mbele katika njia ya ufufukaji.

    Vyombo vya habari vya kimataifa vinaona kuwa ufufukaji endelevu wa uchumi wa China pia umetoa mwanga kwa uchumi wa dunia unaopita kwenye "wakati wa giza". Shirika la habari la Uingereza Reuters limesema watunga sera duniani wanatarajia ufufukaji mzuri wa uchumi wa China, ili kufufua tena mahitaji sokoni.

    Wakati huohuo ukuaji wa uchumi wa China bado unakabiliwa na changamoto nyingi. Gazeti la Nikkei Asian Review la Japan linaona kuwa uchumi wa China utadumisha ukuaji katika siku zijazo, lakini pia utakabiliwa na changamato kubwa zinazotokana na kudhoofika kwa mahitaji kwenye soko la dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako