• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TANZANIA: SABABU YA KUONGEZEKA KWA VITUO VYA MAFUTA

    (GMT+08:00) 2020-10-21 18:10:58

    Imeelezwa kuwa ongezeko la shughuli za kiuchumi na mtandao wa barabara nchini Tanzania, umechangia vituo vya mafuta kuongezeka kwa asilimia 9.32.

    Kwa mujibu wa mkurugenzi wa idara ya Petroli wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma ya Nishati na Maji (EWURA), Gerald Maganga, hadi kufikia Desemba 2019, idaid ya vituo vya mafuta vinavyofanya kazi ilifikia 1,596 kutoka 1,460 kwa mwaka wa 2018.

    Alisema taarifa ya utendaji wa sekta iliyotolewa hivi karibunina mamlaka hiyo, inaonyesha ongezeko hilo ni la asilimia 9.32. Kuongezeka kwa vituo hivi kumechangiwa na ongezeko kubwa la mahitaji ya mafuta.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako