• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Man United yaanza vizuri michezo ya hatua ya makundi kombe la klabu Bingwa.

    (GMT+08:00) 2020-10-21 18:34:43

    OLE Gunnar Solskjaer, Kocha Mkuu wa Manchester United amesema kuwa walistahili ushindi usiku wa kuamkia leo mbele ya PSG kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati wakiibamiza mabao 2-1 PSG. Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Parc des Prinnces jumla yalifungwa mabao matatu yote yalifungwa na wachezaji wa timu ya Manchester United. Bruno Fernandes alianza kufunga bao la kwanza dakika ya 23 kwa mkwaju wa penalti likasawazishwa na Anthony Martial aliyejifunga dakika ya 55 na nyota wa mchezo huo Marcus Rashford alifunga bao la ushindi dakika ya 87. Solskjaer ambaye alianzisha kikosi chake bila nahodha Harry Maguire pia alimuweka benchi kiungo Paul Pogba, na amesema kuwa anahisi vizuri kwa timu yake kushinda na walistahili kupata ushindi huo. Mechi nyingine za michezo hiyo zinaendelea leo ambapo kwa Uingereza Liverpool watakuwa ugenini kukutana na Ajax, Man City wanawakaribisha Porto.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako