• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kuna uwezekano wa Al Ahly na Zamalek kukutana kwenye dabi ya Cairo CAF

    (GMT+08:00) 2020-10-21 18:35:04

    Ushindi wa goli moja iliyupata Zamalek ya Misri katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ugenini juzi dhidi ya mabingwa wa Ligi Kuu ya Morocco Jumamosi wapinzani wakubwa wa Zamalek, Al Ahly nao walitanguliza mguu mmoja katika fainalib ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya Wydad Casablanca katika mechi ya nusu fainali iliyopigwa Uwanja wa Mohamed V jijini Casablanca, Morocco. Wafungaji wa mabao hayo, walikuwa Mohamed Magdi Afsha dakika ya nne na Ali Maaloul dakika ya 62 kwa penalti .Lakini usiku wa kuamkia jana, Zamalek nayo ikiwa katika uwanja huo huo wa Mohamed V nchini Morocco, iliwazamisha Raja Casablanca kwa bao hilo pekee lililopatikana kupitia kwa Mmorocco mwenzao, Achraf Bencharki anayeichezea klabu hiyo ya Misri. Nyota huyo wa zamani wa Wydad Casablanca, alifunga bao hilo pekee dakika ya 18 akimalizia pasi ya Ahmed Sayed 'Zizo', hivyo timu hizo mbili za Misri, Al Ahly na Zamalek sasa zinahitaji sare ya aina yoyote ama ushindi katika mechi za marudiano zitakazopigwa Jumamosi na Jumapili ili kutinga fainali. Zote zikipata ushindi, basi Dabi itafanyika Cairo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako