• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ripoti yaonesha moja ya sita ya watoto duniani wanaishi katika hali ya ufukara

    (GMT+08:00) 2020-10-21 18:42:00

    Ripoti kutoka Benki ya Dunia na Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF inaonesha kuwa, kabla ya kutokea kwa janga la COVID-19, miongoni mwa kila watoto 6 duniani, mmoja anaishi katika hali ya ufukara.

    Ripoti hiyo imeonesha kuwa mwaka 2017 kulikuwa na watoto milioni 356 duniani wanaoishi katika hali ya ufukara ambao gharama ya maisha yao kwa kila siku haikuzidi dola za kimarekani 1.9 na theluthi mbili kati yao wako kwenye eneo la Afrika kusini mwa Sahara. Pia ripoti hiyo imesema kutokana na janga la COVID-19, mwelekeo wa kuwaondoa watoto hao kwenye umaskini haukuweza kudumishwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako