• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 11 wauawa na 13 wajeruhiwa kwenye tukio la kukanyagana katika mji wa Jalalabad, Afghanistan

    (GMT+08:00) 2020-10-21 19:14:33

    Watu 11 wamekufa na wengine 13 wamejeruhiwa katika tukio la kukanyagana lililotokea katika mji wa Jalalabad wa jimbo la Nangahar nchini Afghanistan.

    Maelfu ya watu walikusanyika kwenye uwanja wa mpira karibu na konseli ya Pakistan wakiwa wanaomba visa. Hali ilishindwa kudhibitiwa na matokeo yake ni kuwa watu 11 wamekufa ikiwa ni pamoja na wanawake na watoto, wengine 13 wakiwa ni pamoja na wanawake 10 na wanaume watatu wamejeruhiwa.

    Pakistan iliacha kutoa visa tangu mlipuko wa virusi vya Corona ulipotokea, na huduma ya visa imerudishwa wiki iliyopita. Baada ya huduma kurudishwa maelfu ya waafghanstan kutoka majimbo ya mashariki wameomba visa kwenda Pakistan kuwatembelea ndugu na kutafuta matibabu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako