• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNCTAD lasema biashara ya dunia kupungua kwa kati ya asilimia 7 na 9 mwaka huu

    (GMT+08:00) 2020-10-21 19:14:55

    Ripoti ya Umoja wa Mataifa imekadiria kuwa thamani ya biashara ya dunia kwa mwaka huu itapungua kwa kati ya asilimia 7-9, licha ya kuwepo kwa dalili za ufufukaji dhaifu katika robo ya tatu ya mwaka huu, ukiongozwa na ufufukaji wa China.

    Biashara ya dunia imeonekana kurudi katika hali ya kawaida, lakini bado iko kwenye hali hasi, isipokuwa kwa China. Ripoti imesema katika robo ya tatu ya mwaka huu uuzaji nje wa China uliongezeka kwa nguvu baada ya kupungua katika miezi ya mwanzo, na kuwa na ongezeko la asilimia 10 la mwaka hadi mwaka.

    Mchumi wa Shirika la Umoja wa mataifa la Biashara na Maendeleo UNCTAD Bw. Alessandro Nicita amesema takwimu za biashara za China katika robo ya tatu zimekuwa nzuri, na kama hali ikiendelea hivi China inaweza kuwa na rekodi nzuri ya ongezeko la biashara kwa mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako