• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yahimiza Marekani kuacha ubaguzi dhidi ya wanafunzi wa China

    (GMT+08:00) 2020-10-21 19:55:19

    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Zhao Lijian amehimiza Marekani kuacha ubaguzi dhidi ya wanafunzi na wataalam wa China walioko nchini Marekani.

    Bw. Zhao amesema Marekani imetumia vibaya nguvu ya kimahakama kuwasumbua, kuwahoji, na hata kuwakamata na kuwashtaki wanafunzi wa China nchini humo kwa madai ya uwongo. Amesema kuanzia mwezi Mei hadi Septemba, karibu wanafunzi 300 wa China walipata usumbufu mkubwa katika uwanja wa ndege, kutoka kwa maafisa wa sheria wa Marekani walipokuwa wakiondoka nchini humo, na simu zao za mkononi, kompyuta, na vitu vingine vilichunguzwa vibaya na hata kuchukuliwa.

    Amesema kitendo hicho cha Marekani kinakiuka haki na maslahi halali ya Wachina hao, na kinadhoofisha mawasiliano ya kiutamaduni na ushirikiano wa kielimu kati ya nchi hizo mbili.

    Alipozungumzia China kushiriki kwenye Mpango wa Utekelezaji wa Chanjo dhidi ya COVID-19, amesema madhumuni ya China kufanya hivyo ni kuhakikisha nchi zinazoendelea zinapaa chanjo hiyo.  

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako