• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya watu waliokufa kutokana na ajali ya kuanguka kwa kanisa nchini Ghana yaongezeka na kufikia 7

    (GMT+08:00) 2020-10-21 19:55:59

    Idadi ya watu waliokufa kutokana na ajali ya kuporomoka kwa jengo la kanisa mashariki mwa Ghana imeongezeka na kufikia 7.

    Msemaji wa polisi wa mkoa wa mashariki Bw. Francis Gomado, amesema watu wengine saba wamekuwa wakipatiwa matibabu. Polisi na wanajeshi wanasaidia kazi ya uokoaji, na inaaminika kuwa bado kuna watu wamekwama kwenye kifusi.

    Jengo la ghorofa tatu la kanisa la Church of Prosperity liliporomoka jumanne katika mji wa Akyem Batabi, na waumini 65 walikwama kwenye kanisa hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako