• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uamuzi wa Marekani Kuiondoa Sudan kwenye orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi utaleta athari chanya

    (GMT+08:00) 2020-10-22 09:09:18

    Wachambuzi wa Sudan wamesema Uamuzi wa Marekani kuiondoa Sudan kwenye orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi utaleta athari chanya kisiasa, kiuchumi na kijamii.

    Akiongea na Shirika la Habari la China Xinhua, mtaalamu wa mambo ya uchumi na mhadhiri wa kozi ya uchumi katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Afrika Mohamed Al-Nayer amesema hatua hiyo itatandaza njia kwa sekta ya benki ya Sudan kushughulika na benki za dunia, na kuweza kuomba kupunguziwa madeni yake ambayo kwa sasa ni kiasi cha dola milioni 60 za kimarekani na nchi itanufaika na Mpango wa Kuondoa madeni kwa nchi Masikini katika hatua ijayo.

    Naye mchambuzi wa mambo ya siasa wa Sudan Abdul-Rahim Al-Sunni amefafanua kuwa mazungumzo ya mara kwa mara yanayofanywa na viongozi muhimu wa serikali ya mpito ya Sudan yanaonesha hakuna uhusiano kati ya kufanya uhusiano wa Sudan na Israel uwe wa kawaida na kuondolewa Sudan kwenye orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi, lakini amesema inaonekana kama uhusiano huo upo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako