• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • EAC yatoa wito wa kuendeleza mikakati ya uchumi wa kibaiolojia katika kanda yake

    (GMT+08:00) 2020-10-22 09:09:46

    Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC jana ilitoa wito wa kukuza mikakati ya uchumi wa kibaiolojia katika kanda hiyo ili kutoa fursa ya ushirikiano wa kiutafiti.

    Naibu Katibu Mkuu wa EAC Christophe Bazivamo, amesema mikakati ya uchumi wa kibaiolojia wa kikanda na matumizi endelevu ya rasilimali mbadala za kibaiolojia ili kuzalisha chakula, nishati na bidhaa za viwandani vitapelekea kuhimiza ongezeko la thamani ya biashara kwenye bidhaa za kibaiolojia na huduma. Amebainisha kuwa mkakati huo pia utaongeza juhudi za kikanda katika kushiriki kwa ufanisi zaidi kwenye Eneo la Biashara Huria la Afrika.

    Amewataka wanasayansi, watunga sera na viongozi wa wafanyabiashara kutoa ufumbuzi endelevu wa kibaiolojia ambao utaweza kuchochea ukuaji katika kanda hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako