• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yafikiria kufanya mageuzi ili kuvutia fedha za uwezekezaji kwenye miradi ya miundo mbinu

    (GMT+08:00) 2020-10-22 09:10:09

    Kenya inafikiria kufanya mageuzi kadhaa ya kisheria ili kuvutia fedha za pensheni za ndani na nje ya nchi na kuweza kuwekeza kwenye miradi ya miundo mbinu.

    Katibu wa Wizara ya Fedha ya Kenya Julius Muia amesema serikali imeazimia kuchukua rasilimali za sekta binafsi ili kuziba pengo za fedha za miundo mbinu.

    Muia amebainisha kuwa pensheni ni vyanzo vizuri vya fedha kwa ajili ya miundo mbinu kwa sababu ya kuwepo kwa muda mrefu kwa hiyo ni mali zinazofaa kwenye miradi ya muda mrefu. Amesema serikali inakusudia kutafuta vyanzo anuai vya fedha kwenye miradi ya umma ili kupunguza utegemezi wa vyanzo vya zamani vya kodi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako