• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uingereza yatangaza kurejesha mazungumzo na EU kuhusu uhusiano kati yao katika siku zijazo

    (GMT+08:00) 2020-10-22 09:21:06

    Ofisi ya waziri mkuu wa Uingereza jana ilitangaza kuwa, mazungumzo kati ya Uingereza na Umoja wa Ulaya kuhusu uhusiano kati yao katika siku zijazo yataanza leo tarehe 22, lakini kuna uwezekano wa kutofikia makubaliano.

    Taarifa iliyotolewa na ofisi hiyo inasema, Uingereza iko tayari kuanzisha tena mazungumzo kati yake na Umoja wa Ulaya, na pande mbili zimehakikisha baadhi ya kanuni za mazungumzo. Habari zinasema, kipindi cha kwanza cha mazungumzo kitafanyika tarehe 22 hadi tarehe 25 mjini London.

    Ofisi hiyo inasema, Uingereza na Umoja wa Ulaya zina maoni tofauti katika masuala magumu ya mazungumzo. Lakini pande mbili zinaeleza kwamba inafaa kuwepo juhudi za pamoja ili kufikia makubaliano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako