• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iran yaunga mkono kamati ya katiba ya Syria katika mchakato wa kutimiza amani

    (GMT+08:00) 2020-10-22 09:26:38

    Msaidizi mkuu wa waziri wa mambo ya nje wa Iran anayeshughulikia mambo ya siasa Bw. Ali Asghar Khaji amekutana na mjumbe maalum wa rais wa Russia nchini Syria Bw. Alexander Lavrentiev na kusema, Iran inaunga mkono kazi ya kamati ya katiba ya taifa ya Syria katika mchakato wa amani nchini humo.

    Bw. Khaji amesema, kujenga uaminifu miongoni mwa wajumbe wa kamati hiyo ni msimamo wa kismingi wa Iran.

    Habari zinasema, maofisa hao wawili pia wamejadiliana kuhusu maendeleo mapya ya suala la Syria yakiwemo mchakato wa kisiasa kwenye mgogoro wa Syria, hali ya Idlib nchini Syria, na hali ya uchumi na haki za binadamu nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako