• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vyombo vya habari na wachumi wa Afrika waona China inaendelea kuongoza ufufukaji wa uchumi wa dunia

    (GMT+08:00) 2020-10-22 17:12:31

    Mwelekeo mzuri wa ukuaji wa uchumi wa China katika robo ya tatu ya mwaka huu unaendelea kupongezwa na vyombo vya habari na wachumi wa Afrika.

    Gazeti la Al-Ahram la Misri limetoa ripoti ikisema uchumi wa China umedumisha ukuaji katika robo ya pili na ya tatu ya mwaka huu baada ya kupungua katika robo ya kwanza ya mwaka, na umekuwa injini kuu ya kuhimiza ukuaji wa uchumi wa dunia. Ripoti hiyo inasema China imechukua hatua madhubuti za kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona na kuharakisha mchakato wa kurejesha uzalishaji mali, na kutoa vifaa tiba na vya kielektroniki vinavyohitajika sana kwenye kipindi cha janga hili kwa nchi na sehemu mbalimbali kote duniani. Makala hiyo pia inakadiria kuwa China itaweka mpango wa 14 wa maendeleo ya miaka mitano kwenye mkutano wa tano wa Kamati kuu ya awamu ya 19 ya Chama cha Kikomunisti cha China utakaofanyika mwishoni mwa mwezi huu, na kuunda muundo mpya wa maendeleo unaohimiza kwa pamoja mizunguko miwili ya ndani na ya kimataifa.

    Gazeti la Nairametics la Nigeria limechapisha makala ikisema uchumi wa China uliongezeka kwa asilimia 4.9 katika robo ya tatu ya mwaka huu, na kuimarisha zaidi mwelekeo wake mzuri wa ufufukaji na kuendelea kuongoza ufufukaji wa uchumi wa dunia. Makala hiyo inasisitiza kuwa China imefanikiwa kudumisha hali nzuri ya ajira, na hivyo kuchochea zaidi matumizi ya ndani.

    Gazeti la Daily Nation la Kenya limeripoti kuwa uchumi wa China umerejea kwenye kiwango chake cha kabla ya kutokea kwa janga la virusi vya Corona, na China inatarajiwa kuwa nchi pekee yenye uchumi mkubwa duniani inayodumisha ukuaji chanya mwaka huu. Gazeti hilo limesema, Maonesho ya tatu ya Bidhaa za Kimataifa ya China CIIE yatakayofanyika hivi karibuni mjini Shanghai yamedhihirisha kuwa China ina imani ya kurejesha shughuli kubwa za kiuchumi baada ya kushinda janga la virusi vya Corona, na kuonesha ustahimilivu na uhai wa uchumi wa China, na pia yamethibitisha ahadi makini ya China ya kufungua mlango wake na kuunga mkono kithabiti utaratibu wa pande nyingi. Gazeti hilo limetoa wito kwa wafanyabiashara wa Kenya kutumia fursa ya maonesho hayo kupanua uuzaji nje kwa China, ili kuusaidia uchumi wa Kenya uweze kufufuka mapema baada ya janga la virusi vya Corona.

    Akizungumzia sababu za kufufuka kwa haraka kwa uchumi wa China, Naibu mkurugenzi mkuu wa Kitengo cha mambo ya Asia na Mashariki ya Kati cha wizara ya mambo ya nje ya Afrika Kusini Bw. Anil Sooklal, amesema kwa upande mmoja, janga la virusi vya Corona limedhibitiwa haraka nchini China kutokana na hatua madhubuti zilizochukuliwa na serikali na mshikamano wa watu wa China, kwa upande mwingine, muundo mpya wa maendeleo uliowekwa na serikali ya China na sera zake za kiuchumi za kuhimiza ajira na kuongeza mapato ya wananchi, vimesaidia kuimarisha imani ya wateja na kuhimiza zaidi ufufukaji na maendeleo endelevu ya uchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako